Wakitoa kilio chao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, wakazi wa kijiji hicho wameiomba Serikali kuipatia umeme jua zahanati hiyo ili kuwaondolea adha wajawazito.
Mmoja wa wakazi hao, Ferista Mahangi alimueleza Mwanri anayefanya ziara ya kuhimiza kilimo mkoani Tabora kuwa hali hiyo inahatarisha usalama wa mama na mtoto kwa kupoteza maisha.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Mwajuma Salum ameuomba uongozi wa Serikali mkoa kukisaidia kijiji hicho kupata huduma ya mawasiliano ya simu ili kuwarahisishia kutoa taarifa za upatikanaji wa huduma wakati wa dharura.
Akijibu maombi ya wakazi hao, Mwanri amesema ofisi yake itatafutia ufumbuzi changamoto na kuahidi kukutana na kampuni za simu kuzishawishi kujenga minara ya mawasiliano kijijini hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli ameahidi kupeleka umeme wa sola katika zahanati hiyo ili kuwaondolea adha ya kutumia mwanga wa tochi wagonjwa wakiwamo wajawazito wanahudumiwa usiku.
No comments:
Post a Comment