Wednesday, 16 November 2016

TATIZO LA MINYOO KWA WATOTO



Tatizo la minyoo huwapata watoto na watu wazima.Kwa watoto chini ya miaka 5 wanasumbuliwa sana na minyoo,  hatari kubwa ya kupata minyoo kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja ni  pale wanapoanza kutambaa/kutembea.


Wanaokota vitu vichafu na kuweka mdomoni ,uchafu huo unaweza kuwa na minyoo au vimelea vya minyoo itakayo kwenda mshambulia mwilini.Minyoo ina aina tatu.
1.Tapeworms wanaweza ishi ndani ya mwili wa binadamu wana nyonya damu na kuadhiri organs. 2.Roundworms  hawa wanapatika kwenye udongo na maji wanaweza mwingia binadamu mwili kupitia ngozi wanapitia miguuni pia..3. Flukes nao wanamwingia binadamu kupitia ngozi.

VYANZO VYA MINYOO KWA MTOTO:
  • Mtoto kutambaa au kucheza kwenye udongo wenye minyoo au vimelea vya minyoo.
  • Kutembea miguu peku na kukanyaga uchafu au udongo wenye minyoo.
  • Kuchezea maji machafu au mitaro.


Kula vyakula visivyoiva vizuri kama nyama na samaki sababu zinabeba minyoo.

  • Kunywa maji yasio chemshwa.
  • Kula matunda bila kuoshwa kwa maji safi.
  • Kuoga au kuogelea kwenye maji machafu (mito,habari,maziwa).
  • Uchafu wa choo

DALILI ZA MTOTO MWENYE MINYOO:


  • Upungufu wa damu mwilini_ukiona mtoto anapata tatizo hili jaribu apimwe minyoo.
  • Kutapika mara kwa mara-minyoo inamsababishia kichefu chefu.
  • Kukosa hamu ya kula.
  • Kukohoa mara kwa mara .
  • Hupata homa,
  • Kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa.
  • Kuhara.
  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
  • Maumivu ya kichwa  kuambatana macho kuuma.
  • Kukosa choo (constipation)
  • Tumbo la mtoto kuvimba na kuwa kubwa sababu minyoo huzaliana na kukaa kwenye utumbo mdogo.

MADHARA YA MINYO KWA MTOTO:


Minyoo inamadhara mengi kwa mtoto ,mzazi unapoona hizo dalili vizuri uwahi hospitali .Minyoo husababisha,
  • Utapiamlo.
  • Upungufu wa damu mwilini.
  • Husababisha kifo.
  • Upofu
  • Kudumazwa ukuaji Wake.
  • Huadhiri organs za mtoto.


NJIA ZA KUEPUKA KUPATA MINYOO KWA MTOTO:


Minyoo inaweza kuepukwa kwa njia nyingi cha kwanza mzazi unatakiwa kuwa msafi kwa mzingira mnayoishi na mtoto na njia nyinginezo,
  • Ukipika chakula kama samaki au nyama hakikisha kinaiva vizuri.
  • Chemsha maji ya kunywa.
  • Osha matunda kwa maji safi kabla ujampa mtoto.
  • Mtoto abadilishwe diaper au nepi kila baada ya masaa mawili.
  • Mkate kucha mtoto sababu zikiwa ndefu nirahisi kuhifadhi uchafu na vimelea vya minyoo kuzaliana na kudhuru kwa urahisi.
  • Mikono ya mtoto isafishwe kabla ya kula na baada.
  • Atumie sabuni na maji safi kuosha mikono baada ya kutoka chooni.


Usafi wa choo au Poti anayo tumia mtoto ni muhumu kuosha vizuri , kubadili maji safi na kuosha ndoo  mnayotumia choo kila siku.

TIBA:


Mzazi unatakiwa kumpa mtoto dawa za minyoo kila baada ya miezi 3 mfano Mebendazole au Albendazole.  Dawa hutolewa kuzingatia vipimo na umri wa mtoto ,soma maelezo uliopewa na dakatari au duka la dawa kabla hujampatia mtoto.  Unatakiwa uandike sehemu tarehe na mwezi uliompa dawa ili baada ya miezi 3 ijayo utajua mara ya mwisho ulimpa lini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!