Thursday, 10 November 2016
Rais Magufuli amtembelea Mke wake na Wagonjwa wengine Waliolazwa Muhimbili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mke wake, Mama Janeth Magufuli aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili akipatiwa Matibabu. leo Novemba 10,2016
Rais Magufuli akiongea na wagonjwa mbali mbali katika Hospitali ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya Madaktari na Wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
======
Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli, Janeth, amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Ikulu imetoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji.
Hata hivyo, haijasema anaugua wapi.
Novemba mwaka jana, siku chache baada ya kuapishwa hospitali hiyo ni miongoni mwa taasisi za serikali ambapo Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza.
Alisema alisikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.
Alidha, alipata hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi na mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi kadha.
Alibadilisha usimamizi wa hospitali hiyo.
Taarifa ya ikulu inasema leo, alipokuwa anamjulia hali mkewe, pamoja na mke wa balozi na waziri mstaafu wa Tanzania Omar Ramadhan Mapuri, wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji wamemshukuru "kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili na wamebainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, pia wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.
Chanzo: BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment