Moto mkubwa ambao umekuwa ukiwaka kwa siku kadha Israel sasa unakaribia mji wa Haifa kaskazini mwa nchi hiyo. Moto huo umesababisha uharibifu mkubwa. Watu karibu 50,000 katika mitaa minane wametakiwa kuhama, maafisa wanasema.
Hakujaripotiwa taarifa zozote za watu kuumia vibaya lakini watu kadha wamepelekwa hospitalini wakikabiliwa na matatizo kutokana na kupumua hewa iliyojaa moshi.
Ukosefu wa unyevu kwenye hewa pamoja na kuwepo kwa upepo mkali kumesababisha moto huo kuenea upesi.
Ndege iliyobebea maji ya kuzima moto ilipaa juu ya mji huo. Polisi wanasema wakazi wamekabiliwa na moto kutoka maeneo manne.
Katika baadhi ya maeneo ya Haifa, moto huo umeanza kukaribia sana majumba ya makazi.
Maeneo yanayokabiliwa na moto huo yalikuwa yamekabiliwa na kiangazi kwa miezi miwili. Mawaziri wanasema huenda moto huo uliwashwa makusudi.
Moto huo hapa unaonekana ukiwaka karibu na barabara kuu ya Route 1 inayounganisha Tel Aviv na Jerusalem.
Maelfu ya wakazi wamehama makwao Haifa, wakijaribu kunusuru mali yao.
Wazimamoto wanaendelea na juhudi za kukabiliana na moto huo, ingawa umeathiri maeneo makubwa na wazimamoto hao ni wachache. Wanahitajika pia kuwalinda raia na nyumba zisishike moto.
Moshi kutoka kwa moto huo Haifa wakati mwingine ulikuwa mwingi kiasi kwamba karibu jua lizibwe.
Misitu iliyo karibu na Jerusalem pia inatishiwa. Israel imepokea usaidizi kutoka Urusi, Uturuki, Ugiriki, Italia, Croatia na Cyprus.
No comments:
Post a Comment