Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Serikali imesema kuwa licha ya Mipango mikakati na mbinu madhubuti ambazo zimetekelezwa bado takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi miongoni mwa makundi maalum na yale yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU yapo juu.
Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto ambapo imesema ilianza kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa makundi hayo maalum tangu mwaka 2010 baada ya kufanya tafiti na kugundua kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kiko juu kwenye makundi hayo.
Serikali imeyataja makundi yaliyopo hatarini zaidi kwa maambuki hayo ni pamoja na wasichana na wavulana, walio katika umri wa balehe, watoto yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi, wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya ngono kinyume na maumbile, watu wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano.
Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu 1,400,000 wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo, watu 839,574 wanapatiwa tiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU zinazotolewa katika vituo ambapo takriban vituo 4,000 vilikuwa vinatoa huduma hiyo nchi nzima hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu (2016
No comments:
Post a Comment