
Siku kadhaa zilizopita nikiwa nyumbani nimetulia mida ya saa mbili usiku nikasikia kengele inalia getini.Dada akaenda kufungua na akaja kuniambia kuwa nina mgeni wangu nje.Nikajiuliza nani huyu mida hii usiku?maana najua miaka hii mtu kuja kwako lazima atakuwa kawasiliana na wewe kabla.
Basi nikatoka nje nikamkuta mama flani hivi.Nikamsalimia huku nikimtazama usoni nikihisi sura kama naijua ila sina hakika.Basi akaniambia najua unaweza kuwa umenisahau ila mie nakumbuka mwakauliopita niliwahi kupita hapa kwako nikiwa naumwa.Sikuwa na kujua wala hunijui ila sikuwa na pesa yoyote kwa ajili ya kwenda hospital nikakugongea ukanifungulia nikakueleza shida yangu ukanisikiliza na ukanisaidia japo hunijui.Nikamwambia kweli nimekukumbuka akasema unaweza kuwa umesahau sababu nilikuwa dhoofu sana hapa nimenenepa.Mimi nakaa mtaa wa tatu kutoka hapa kwako niliweka nadhiri nitarudi tena kukushukuru na kukusalimia.
Akaniambia wakati nakuja hapa sikujua kama wewe ni Dina Marios nimekuja kujua miezi ya hivi karibuni.Mdogo wangu nikwambie...mimi nilitokea familia ya kujiweza,nilisoma shule nzuri mpaka elimu ya juu.Usichana wangu nilikuwa moto moto hakuna asonijua hakuna kiwanja sijaenda kujiachia.Nilikuwa naimba mziki band flani hivi Hata radio flani maarufu jingle yake ambayo ipo mpaka leo ile ni Sauti yangu mimi.Ni mambo mengi yalitokea kwenye maisha yangu leo hii nipo hapa Nina miaka 49 ni kama nina miaka 60 nimezeeka.Sina meno mdomoni (akifungua kinywa chake) Yote haya ni maisha tu.
Mdogo Wangu endelea kuwa na upendo watu wanapokuombea mema dua na sala zao Mungu anazisikia na ni Kinga yako.
Mdogo Wangu kuwa makini na marafiki maana adui yako ni mtu wa karibu yako sana wala hatoki mbali.
Mdogo Wangu utumie vizuri wakati wako huu maana utakuja kupita.Na hakikisha ukipita umepata mafunzo mengi na si majuto.
Mdogo Wangu katika maisha haya usije ukaumiza watu wanaokupenda na kukujali.Ni dhambi kubwa sana kuumiza watu wasio na hatia zaidi wanakuwazia mema.
Mdogo Wangu wakati huu utapita hakikisha unaacha kumbukumbu njema kwa wale wanaokupenda na kukujali.
Mdogo Wangu hakikisha unajiweka karibu na Mungu hivi sasa ukiwa kijana sio hapo baadae.
Basi tukaagana na mgeni wangu..!
Basi tukaagana na mgeni wangu..!













No comments:
Post a Comment