Monday 31 October 2016

TANZIA: BONDIA MAARUFU NCHINI THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA


TANZIA Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kupigwa vibaya na watu wasiojulikana maeneo ya Kimara jijini Dar essalaam.

Mzee Malifedha Christopher Mashali baba Mzazi wa Thomas Mashali ambaye ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo huko Kimara jijini Dar es Salaam amefunguka na kuelezea kilichomkuta mwanaye.
Malifedha amesema kuwa yeye mwenyewe amepata taarifa ya kifo cha mwanaye huyo baada ya kundi la vijana kuja kwake usiku wa saa tisa na kumpa taarifa kuwa Mashali ameuawa na watu wasiojulikana.
Akiongea kwenye kipindi cha SupaMix mzee Malifedha amesema kwa taarifa alizopata ni kwamba mwanaye alipigwa sana jambo ambalo lilifanya mpaka ubongo kutoka kichwani. 
"Mashali ni mtoto wangu wa tano yeye alizaliwa mwaka 1980 mwezi sikumbuki, ameacha watoto kama watano hivi wengine huko pembeni siwezi kujua. Mimi nilikuwa nyumbani nimelala kwenye saa tisa hivi usiku walikuja vijana hapa walinigongea sana mlango sikutaka kufungua nilijua polisi. Wamegonga sana na kupiga mateke nikawaambia vijana vipi wakasema sisi tumekuja hapa kukupa taarifa kuwa Mashali amefariki amepigwa vibaya sana na wamempasua sana kichwa, mpaka ubongo umetoka amepelekwa hapa Sinza Palestina. Ikabidi niwaamshe dada zake wakaenda Palestina wakaambiwa ameshapelekwa Muhimbili na walipofika huko kweli wakakuta mambo yameharibika" Mzee Malifedha 
Chanzo:ETV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!