Timu inayoundwa na Wana-Diaspora wa Kitanzania waishio Sweden, Kilimanjaro FC, hivi karibuni imefanikiwa kupanda daraja kutoka Daraja la Saba kwenye Ligi ya Sweden ijulikanao kama Allsvenska na kufikia Daraja la Sita.
Bwana Abdul Njaidi ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bwana Adam Maingu, umeipongeza timu hiyo ya Kilimanjaro FC kwa hatua hiyo kubwa na ya kutia matumaini katika kuinua soka la nchi yetu kwa ujumla.
"Vijana wa Kilimanjaro FC wamekuwa mabalozi wazuri kwenye kuitangaza nchi yetu kimataifa. Sisi wa PSPF tunawakaribisha vijana wa Kilimanjaro FC na Watanzania wengine walio nje ya nchi kujiunga na mifuko yetu ya hifadhi kwa kuwasaidia wao wenyewe na ndugu na jamaa zao walio nyumbani." Anasema Bw. Abdul Njaidi akiongea na mtandao wa Mjengwablog.com
No comments:
Post a Comment