Sunday, 16 October 2016

Mbatia: Uhakiki wa vyeti feki uanzie kwa Rais na viongozi wengine



Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia ameshauri zoezi la ukaguzi wa vyeti feki vya kitaaluma linaloendelea lianzie kwa viongozi wakubwa Serikalini.



Mhe. James Mbatia (MB) Vunjo, na Mwenyekiti Taifa NCCR. Ametaka zoezi la uhakiki wa vyeti feki ni vyema likanzia kwa Rais na viongozi wengine.

Binafsi naunga Mkono hoja ya Mhe.Mbati kwa sababu mbili tu.

1.Kiongozi hutakiwa kuongoza kwa Mfano, tulitegemea akianza Rais, watafuata na viongozi wengine wote, PM, VP, W. N/W, RC, DC, Wabunge hadi Madiwani.

Aidha, kuna mazoezi mengi hapo awali yalianzishwa na Rais na viongozi wengine Tuliona wakati wa kampeni mbalimbali kama vile UKIMWI na Malaria No More, Tuliona Utambulisho wa anuani za makazi, Tuliona kwenye BVR na NIDA.

Ikumbukwe kuwa, JPM alikuwa mastari wa mbele, kwa maana wa kwanza katika Zoezi la UHAKIKI WA SILAHA Mkoa wa Dar.

2. Kuonyesha uhalali wa zoezi husika, kuwa kama zoezi likianza na Viongozi mara nyingi huchukuliwa ni serious na ni zoezi halali lisilo la kibaguzi kwa baadhi ya kada tu.

Kwani Mpaka sasa kuna baadhi ya Mawaziri inasemekana wanatumia majina fake, so uhalali wa zoezi hili upo wapi?

My Take:
Zoezi lianze kusafisha Nyumbani kwanza ( Baraza la Mawaziri & vigogo)

Source: Gazeti la Mtanzania.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!