Saturday, 29 October 2016

MAPISHI YA LEO! KEKI


Mahitaji:
Unga wa ngano vikombe 2¾

Sukari kikombe 1½
Baking powder kjk 1 chakula
Chumvi ¼ kjk chai
Siagi kikombe 1
Maziwa fresh kikombe 3/4
Maziwa fresh 1/4 kikombe
Mayai 4
Vanilla vjk 2 chai


Maelekezo:-
1.Washa oven joto 180°c. Katika bakuli changanya vitu vikavu vyote.
2.Tia siagi na maziwa 3/4 kikombe, piga hadi vichanganyike
3. Katika bakuli nyingine piga mayai,maziwa yaliyobaki na vanilla.
5. Taratibu tia katika mchanganyiko wa unga na piga kwa dk 1 kuchanganya .
6. Tia katika chombo cha kuokea, oka kwa muda wa dk 30-35 hadi kijiti ukitia kati kitoke safi.
7. Acha keki ipoe. Keki tayari kwa kula au weza pamba na icing upendayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!