CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefuta maandamano yaliyopangwa kufanyika leo nchi nzima, yaliyolenga kuendeleza harakati za Umoja Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).
Kutokana na kufuta maandamano hayo, Chadema imesema itafanya ziara katika kanda na mikoa ya kichama na vikao vya kisiasa nchini kuendeleza azma hiyo. Pia imesema itafanya ziara nje ya nchi kuelezea jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya kisiasa nchini, ili kujenga shinikizo la kidiplomasia dhidi ya serikali.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea mikakati na mapendekezo yaliyotolewa na kamati maalum ya kamati kuu iliyokutana juzi, kujadili hali ya kisiasa na kupokea taarifa kuhusu jitihada za viongozi wa dini, waliopanga kukutana na Rais John Magufuli.
NIPASHE.

No comments:
Post a Comment