Mama mjamzito anapopitiliza siku za kujifungua kwenye wiki ya 40 ,anakosa amani na kujiuliza maswali mengi.Mimba ikifika week 41-42 hapo inakuwa overdue. Kuna sababu tofauti zinazo pelekea mama kupitiliza siku zake za kujifungua.
Baadhi ya sababu za overdue
:Iwapo mama atahesabu siku zake vibaya basi hapo ataona amepitiza siku za kujifungua
:Kama ulishazaa kwa mara ya kwanza na ukapitili
za basi uzao wako unaofata tatizo linaweza kujirudia
:Kupitiliza kujifungua huridhishwa kupitia wanafamilia
:Watoto wa kiume huchelewa kutoka tofauti na wakike
:Matatizo ya kondo la uzazi kushindwa fanya kazi ipasavyo
Mama anapo overdue anakuwa anakosa raha,mwili kuchoka,anashindwa kulala ,anapata kiungulio na kukosa choo.
MADHARA YATAKAYOJITOKEZA MAMA ANAPOPITILIZA SIKU ZA KUJIFUNGUA:
Mimba inapokuwa zaidi week ya 41 kunakuwa na hatari kwa afya ya mtoto
:Mtoto anaweza kupata choo (kunya) na kula kinyesi akiwa tumboni
:Kupungua kwa kiwango cha maji yanayomzunguka mtoto (ambiotic fluid)
:Mapigo ya moyo ya mtoto kupungua
:Mama anauwezo wa kuzaa kwa c-section sababu mtoto kesha kuwa mkubwa
NINI MAMA ANATAKIWA KUFANYA:
Mama anapopitiliza kujifungua anahitaji kuwa karibu na daktari mara kwa mara na iwapo ukapata dalili yoyote usioielewa wahi hospital.inaweza kuwa kifafa cha uzazi au tatizo lolote kubwa.
Mimba inapokuwa week ya 42 -43 vizuri daktari apime mapigo ya moyo ya mtoto,kuangalia kucheza kwa mtoto na kiasi cha maji maji yaliopo(amniotic fluid) sababu yanapo pungua husababisha mtoto kunyong’wa na umbilical cord shingoni.
Mimba haiwezi kaa kwa muda mrefu, iwapo hatopata uchungu daktari atamwanzishia uchungu ili njia ifunguke na iwapo itashindikana basi atapasuliwa.
Note:
Kuna wanawake wengine njia zao za uzazi haziwezi tanuka zimeumbwa ndogo sana, hata wawekewe uchungu kwa muda mrefu bado lazima wazae kwa upasuaji .Ni vizuri ukazalishwa na daktari aliekuzalishwa mwanzo sababu anajua historia yako ya uzazi iwapo ni uzazi wako wa pili au zaidi.
SHUKRAN KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO
No comments:
Post a Comment