VIFAA vinavyotumika kuhakiki vyeti kwa watumishi wa umma pamoja na kuandikisha Vitambulisho vya Taifa, ikiwemo kamera zenye thamani ya Sh. milioni sita vimeibiwa na watu wasiojulikana katika jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Kamera mbili na viegesho vyake (stand), vimebainika kupotea jana asubuhi wakati wa kujiandaa kuendelea na kazi ya kuhakiki vyeti na kuandikisha Vitambulisho vya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humu, Nyabaganga Talaba, alithibitisha kupotea kwa kamera hizo za Nida.
“Leo (jana) asubuhi, Ofisa wa Nida alibaini kuwa kamera mbili na viegesha vyake, havionekani. Tunaendelea kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwabaini wahusika na kuvipata vifaa hivyo," alisema Talaba.

No comments:
Post a Comment