Wednesday, 5 October 2016

Hatimaye chanjo zawasili



File Photo
 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema chanjo zilizoadimika nchini, zimewasili na wananchi watapata huduma kuanzia sasa.



Chanjo zilizopungua ni pepopunda (TT) na kifua kikuu (BCG), ambazo imeelezwa zimewasili nchini Oktoba 3 na kwamba, leo itapokea za polio (OPV) ambazo zitasambazwa wiki hii.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja alisema: “Wazazi na walezi wanaombwa kuwapeleka kliniki watoto ambao hawakupata chanjo.”
Aliwahimiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kushiriki vyema katika utoaji wa chanjo hizo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!