Sunday, 23 October 2016

CHAWABATA CHAIOMBA SERIKALI KURUDISHA MUDA WA ZAMANI WA KUFUNGUA BAA NCHINI



Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na  waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. 



Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.  akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein wakati akizungumza na mtandao wa  www.habarizajamii.com Dar es Salaam leo asubuhi  kuhusu changamoto waliyonao wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na vinywaji baridi.

"Tunaiomba serikali kuangalia kwa karibu kuhusu muda wa kufungua baa kwani muda huu wa sasa wa kufungua saa 10 jioni na kufunga saa tano ni mdogo ukilinganisha na ilipokuwa awali wa kufungua wakati wote" alisema Hussein.

Hussein alisema nia ya serikali haikuwa mbaya ya kufungua baa saa 10 lakini hawakuangalia upande wa pili wa wamiliki wa baa hizo kwani wengi wao kwani katika muda huo wengi wao hawafanyi kabisa biashara.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara hao wanahitaji kupata muda wa siku nzima wa kufanya biashara zao ili waweze kumudu kupata fedha za fedha za kulipa kodi ya serikali na mishahara ya wafanyakazi na wahudumu wa baa ambao ni wengi ambapo hivi sasa wanashindwa kufikia malengo.

Alisema baadhi ya baa zimepunguza wahudumu wake kutokana na kubanwa na muda huo ambapo wahudumu wamekuwa wakiingia jioni tu baada ya muda wa asubuhi kupigwa marufuku na serikali.

"Wenye mabaa hivi sasa wapo katika changamoto kubwa ya biashara zao tunaiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa sura nyingine ili kuinusuru biashara hiyo kuanzia mmiliki wa baa na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na serikali yenyewe kupata kodi yake.

Alisema kuwa changamoto hiyo waliibaini baada ya kuzitembea baa kadhaa jijini Dar es Salaam mapema mwezi huu ambapo walipata fursa ya kuzungumza na wamiliki wa baa na wahudumu wa baa hizo.

Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck alisema kutokana na kubanwa kwa muda wa kufungua baa kumepunguza ajira kwa wahudumu wa baa nyingi hapa nchini ambao ni wadau wao wakubwa wa viwanda vya bia na wamiliki wa baa.

Alisema bila ya wahudumu wa baa biashara hiyo inakuwa inapoteza  kundi muhimu la kuzifanya bia hizo kusambaa katika soko.

"Tunaiomba serikali kuruhusu baa kufunguliwa wakati wote kama ilivyokuwa zamani jambo litakalosaidia wenye mabaa kupata fedha za kulipa mishahara na kodi " alisema Lameck.

Lameck aliongeza kuwa muda uliotengwa na serikali ni kama masaa saba tu kuanzia saa 10 hadi saa tano usiku na ndani ya muda huo wateja wengine wanaondoka kuanzia saa moja hadi saa tatu hivyo kuwa changamoto ya biashara hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)




























No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!