Saturday, 15 October 2016

BONDE LA ISIMILA KATIKA HISTORIA YA ZAMA ZA MAWE-(ISIMILA STONE AGE)






Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa huu wa Iringa.

Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hili ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka 1951. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina ya tofauti ya viboko.
Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.

Chaguo la visu na shoka kutoka mwisho wa Zama za Mawe


Mahali mbalimbali duniani penye mawe ya kufaa wataalamu walitambua mabaki ya karahana ambako visu vya mawe vilitengenezwa kwa vingi. Mfano mmojawapo ni bonde la Isimila karibu na IringaTanzania ambako mabaki mengi ya utengenezaji wa vifaa vimepatikana. Mafundi wa kale walipasua mawe na kuyapigapiga hadi kupata visu vikali. Vipande vidogo vilivyokatwa pamoja na visu visivyoridhika vilitupwa mahali pa kazi na hivyo wataalamu wamepata picha ya kazi zilizotekelezwa. Kwa kutazama mabaki kama yale ya Isimila katika pande zote za dunia inawezekana kupata picha ya maendeleo ya teknolojia ya kutengeneza vifaa vya mawe kwa kupata visu vyembamba na vikali zaidi. Karahana kama Isimila zinaonyesha uzalishaji kwa wingi kwa hiyo ni dalili ya biashara maana wataalamu wanahisi visu hivi vilibadilishwa kwa chakula au chumvi na watu walioishi katika sehemu pasipokuwa na mawe ya kufaa.
Zama za Mawe hupangwa katika vipindi mbalimbali kufuatana na maendeleo ya kuboreshwa kwa vifaa vya mawe ingawa mabadiliko haya yalikuwa tofauti sana kati ya maeneo mbalimbali. Kwa mfano tamaduni za Amerika zilitumia vifaa vya mawe vyenye kiwango cha juu hadi kufika kwa Wazungu katika karne ya 16 ingawa menginevyo wenyeji hao walikuwa na miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya na maendeleo mengine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!