MTU mmoja Mkenya ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kumchoma kisu askari aliyekuwa akilinda ubalozi wa Marekani jijini Nairobi nchini Kenya.
Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Girigiri
katika jijini la Nairobi Vitalis Otieno amesema polisi wamemuua mtu huyo na kwamba, jina lake halitatolewa wakati tukio bado liko wenye uchunguzi.
Amesema lengo la mtu huyo kumshambulia askari bado halijajulikana. Askari alichomwa kisu kichwani.
"Askari alijibu shambulio kujilinda na amefanikiwa kumuua mshambuliaji. Ofisa wangu amelazwa hospitali katika hali imara. Mtu huyo amekufa papo hapo," alisema Otioano.
Taarifa zaidi kuhusu majeraha aliyepata askari huyo hazijafahamika.
Ubalozi wa Marekani umethibitisha kuwa mtu huyo ameuawa nje ya eneo lake na kwamba hakuna mfanyakazi wa ubalozi aliyehusika katika tukio hilo.
Ubalozi wa Marekani uko wilaya ya Girigiri katika jiji la Nairobi ukiwa miongoni mwa balozi kadhaa na ofisi za Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment