Thursday 20 October 2016

Akon azuru Liberia kuweka umeme katika shule 2

Mwanamuziki wa mtindo wa Hip Hop azuru nchini LiberiaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMwanamuziki wa mtindo wa Hip Hop azuru nchini Liberia
Mwanamuziki wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Akon yuko ziarani nchini Liberia kuweka umeme wa jua katika shule mbili za msingi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.


Ni miongoni mwa miradi yake ya kuwawekea umeme watu milioni 600 katika bara la Afrika.
Akon ambaye ni mzaliwa wa Senegal anashirikiana na kampuni ya Bridge International Academies pamoja na ushirikiano na mashirika mengine ya kimatifa kusimamia shule 50 nchini Liberia.
Wakati msafara wake wa magari ulipokuwa ukipita katika mji mkuu wa Monrovia,chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi,mwanamuziki huyo alisema kuwa inasikitisha kuona kwamba hakuna umeme katika barabara ya kilomita 50 kutoka uwanja wa ndege.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!