Wednesday, 14 September 2016

Wazee miaka 70 kulipwa pensheni ya 20,000/-


SERIKALI inaandaa mpango wa Pensheni kwa wazee nchini na kwamba kila mzee mwenye umri wa miaka 70 atakuwa akilipwa Sh 20,000.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Antony Mavunde amesema Serikali inaandaa mpango huo na mchakato wake ulishaanza na itakapojiridhisha kuwa taratibu zote ziko sawa itatoa taarifa ya kuanza kutoa malipo hayo.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventura Kiswaga (Chadema), aliyetaka kufahamu lini serikali itaanza kuwapatia kiinua mgongo wazee.
Akijibu swali hilo, Mavunde, amesema katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 na kuwalinda wazee nchini na umasikini wao wa kipato, serikali inaandaa mpango huo.
Mavunde, amesema hadi sasa serikali imetekeleza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuanisha idadi ya wazee wote nchini, kuanisha viwango vya pensheni, kuandaa utaratibu utakaotumika kulipa pensheni, kuandaa taratibu za kiutawala za kusimamia utoaji pensheni kwa wazee na kushirikisha wadau mbalimbali katika kuandaa mpango huo wa pensheni kwa wazee.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!