dc paul makonda akiongoza upimaji wa magojwa ya moyo yaliotolewa bure katika viwanja vya leaders.
UPIMAJI afya bure jijini Dar es Salaam limegubikwa na changamoto ya ukosefu wa baadhi ya vifaa hasa vya vipimo vya figo.
Utaratibu huo uliotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wiki iliyopita, jana uliingia katika siku ya tatu jana.
Wakizungumza na Nipashe jana kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini unapofanyika utaratibu huo, watu waliojitokeza kupima afya walidai kukosa huduma ya kupimwa figo kutokana na kutokuwapo kwa vifaa na watalazimu kwenda hospitalini ambako watalipa gharama kubwa.
Amina Selemani, mkazi wa Magomeni Mapipa, alisema amekosa vipimo hivyo na imemlazimu kurudi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuna bango linaloonyesha kuwapo kwa vipimo vya matatizo ya figo.
“Nimekuja kwa ajili ya kupata vipimo vya figo ambavyo walitutangazia kuwa vipo, lakini nimeingia kwa daktari ananiandikia nirudi hospitalini Muhimbili,” alisema Amina.
Donatus Ngonyani, mkazi wa Yombo Kilakala, aliiomba serikali kujipanga upya kupitia changamoto zilizojitokeza katika utaratibu huo wa kupima afya za watu bila malipo kwa kuwa umewahamasisha wengi.
Alisema utaratibu unapaswa kwenda sambamba na uwapo wa vifaa vya kutosha katika maeneo yanayotengwa ili kuepuka usumbufu kwa wananchi.
“Ni kweli mkuu wa mkoa alikuwa na nia njema kwa sisi wananchi, lakini nashauri lifanyike kila baada ya miezi miwili au mitatu kukiwa na vifaa vyote ili kuepuka usumbufu,” alisema na kuongeza:
“Hali za Watanzania kwa kipindi hiki ni ngumu sana, hawawezi kulipia vipimo hivi, kama wanaamua kutoa huduma basi watoe kila wilaya ili kuondoa msongamano wa watu.”
Baadhi ya wauguzi ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walikiri kuwapo kwa changamoto ya ukosefu wa vifaa vinavyotumika kupima baadhi ya magonjwa ikiwamo figo.
Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ziada Sellah, alisema serikali imejipanga vizuri kuhakikisha zoezi linafanikiwa ingawa idadi ya waliyohudhuria ni kubwa ukilinganisha na siku zilizopangwa.
“Ilitakiwa tumalize zoezi siku ya Jumapili, lakini kutokana na mwitikio kuwa mkubwa, tumeongeza siku mbili zaidi kuhakikisha waliojiandikisha wanapata huduma hii,” alisema.
Sellah alisema serikali ilikuwa na mpango wa kutoa huduma hii kwa wakazi wote. Alisema hadi kufungwa zoezi hili leo, wanatarajia kutoa huduma hiyo kwa watu 11,350 na kwamba watakaa na Mkuu wa Mkoa, Makonda kuangalia kama kuna uwezekano wa kulirudia tena.
Utaratibu huo wa kuwapima afya watu bila malipo, umelenga kuhamasisha wakazi kupima afya mara kwa mara hata kama si wagonjwa.
NIPASHE:

No comments:
Post a Comment