Licha ya serikali kupiga marufuku ya uuzaji wa damu nchini, Ofisi ya Mkuu wa wilaya imedaiwa kubariki uuzaji damu.
Kwa mujibu wa barua ya Agosti 26, mwaka huu, ya kumbukumbu GTA/CHT/AB.69/116/01/137 iliyosainiwa na Ofisa tawala wa wilaya hiyo, Kamugisha J.A, ikimtambulisha Bernard Lukuba (37), mkazi wa kijiji cha Muungano, Chato kuwa ni mgonjwa na asaidiwe pesa ya kununua damu.
Sehemu ya barua ilisema mgonjwa huyo amekuwa akisumbuliwa na upungufu wa damu na mara kadhaa alipata huduma za afya katika Hospitali ya Bukumbi, mkoani Mwanza na Chato, lakini tatizo lake halijatibika na kusababisha kuishiwa nguvu mara kwa mara.
Aidha, kitendo cha ofisi ya DC kuruhusu mgonjwa huyo kuchangisha fedha ya ununuzi wa damu, kimetafsiriwa kuwa ni kupingana na maelekezo ya serikali ya kutaka watu kuchangia damu kwa hiari.
Akizungumza na gazeti hili, Lukuba alisema alilazimika kwenda kuomba msaada wa matibabu kwenye Ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kutokana na ukata wa fedha unaomkabili.
Mkuu wa wilaya hiyo, Shaaban Ntarambe, alipoulizwa kuhusu kibali hicho, alidai mwenye jukumu la kukizungumzia ni Katibu tawala kwa madai ofisi yake ndio iliyotoa barua hiyo.
Aidha, alisema mgonjwa hana kosa kwa kuwa amekabidhiwa nyaraka halali na serikali kwa ajili ya kumsaidia kutatua tatizo lake.
Akizungumzia uuzwaji wa damu, Ofisa mteknolojia maabara mpango wa damu salama, Mkoa wa Geita, Onna Panga, alisema hakuna waraka wowote wa serikali unaoruhusu watu kuuza ama kununua damu.
Alidai tatizo hilo lilipaswa kupelekwa idara ya maendeleo ya jamii katika wilaya hiyo ili kupata usaidizi badala ya kuchangisha fedha za kununua damu.

No comments:
Post a Comment