Picha na Maktaba
Dar es Salaam. Kitengo cha Upasuaji wa Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kesho kinatarajia kuanza awamu ya tatu ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na tatizo la mgongo wazi, wiki inayoanza.
Upasuaji huo unaofanywa na kitengo cha Moi kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM utawafikia watoto zaidi ya 60 katika mikoa mitano.
Kaimu Mkurugenzi wa Moi, Dk Othman Kiloloma amesema lengo ni kuwafikia watoto wengi zaidi iwapo watajitokeza katika mikoa ya Tanga, Moshi, Arusha na Mara ambako huduma hiyo itakuwa inatolewa.
Ofisa habari wa taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba ametoa wito kwa kwa wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo kujitokeza kwa wingi kwa sababu huduma hiyo inatolewa bure na kwamba watoto wakipata matibabu mapema wanaweza kupona
No comments:
Post a Comment