Tuesday, 6 September 2016

MKURUGENZI ILEJE HAJI MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA


 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa  kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.




baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.


Na fredy mgunda,ileje

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.
Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.
“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.
Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi  wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.
Lakini mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!