Mchungaji Dk Getrude Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari nje ya gereza la Keko jijini Dar es Salaam jana.
WAFUNGWA 78 katika magereza matatu jijini Dar es Salaam wameachiliwa huru baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assembles of God (Mlima wa Moto), Dk. Getrude Rwakatare kuwalipia faini ya Sh. milioni 25.
Mmoja kati ya wafungwa hao, amesimulia namna alivyofungwa jela kwa kukosa Sh. 50,000.
Kiongozi huyo wa kiroho akiongozana na waumini wenzake, jana walifika katika Magereza ya Keko, Ukonga na Segerea na kuwalipia fedha na kisha kuondoka na wafungwa 50 kati ya 78 ambao wanatakiwa kuachiliwa huru.
Wafungwa wengine 28 wataachiliwa siku yoyote kuanzia leo kwa kuwa walishindwa kutolewa jana kutokana na kuwapo kwa kasoro ikiwamo kukosewa majina ya wafungwa.
NIPASHE.
No comments:
Post a Comment