SERIKALI ya Japan imeahidi kukarabati shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni.
Ahadi hiyo ilitolewa na Balozi wa Japan nchini,




Masaharu Yoshinda, alipokutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam jana, kuzungumzia maafa yalitokea Kagera.
Tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 ni la ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya majanga hayo kimataifa, na kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa earthquaketrack.com ndilo kubwa zaidi katika historia kutokea nchini.
Aidha, kwa niaba ya serikali ya nchi yake, Balozi Yoshinda ameomba kupatiwa orodha ya mahitaji ya dharura yakiwamo mahema, mablanketi, dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.

NIPASHE.