Thursday, 15 September 2016

Hukumu waliolawiti, kuweka picha mitandaoni Sept 20

Image result for arrested
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imepanga Septemba 20 mwaka huu, kusoma hukumu ya kesi ya kulawiti na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii inayowakabili washitakiwa Erick Kassira (39) na Juma Richard (31).

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, alidai mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo ilitajwa kwa ajili ya hukumu na kwamba upande wa mashitaka ulikuwa tayari kusikiliza hukumu hiyo.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Said Mkasiwa, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 20 mwaka huu, kwa kuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo.
Upande wa mashitaka katika kesi hiyo, ulifunga ushahidi kwa kuleta mahakamani mashahidi wanne pamoja na vielelezo, zikiwemo picha za tukio, ambapo baadaye washitakiwa walikutwa na kesi ya kujibu na walijitetea.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Agosti 23, 2014 kwenye maeneo ya Maembe Bar & Guest House, iliyopo Kiwalani Yombo, wilayani Ilala, Dar es Salaam washitakiwa walimkuta mlalamikaji akiwa na Sanifa Bakari katika chumba namba sita ambaye walidai kuwa ni mke wa Kassira hivyo, kudai kuwa wamemfumania mlalamikaji.
Kutokana na hali hiyo, washitakiwa hao walimtaka mlalamikaji kutoa kila alichonacho ambapo aliwakabidhi kompyuta aina ya HP ya thamani ya Sh 350,000, fedha taslimu Sh 100,000, simu aina ya Tecno ya thamani ya Sh 350,000 pamoja na viatu.
Ilidaiwa kuwa, baada ya kukabidhiwa vitu hivyo, walimlawiti na kumpiga picha huku wakiwa utupu na kumtaka waandikishiane kutoa Sh milioni moja ili wasitume picha hizo kwenye mitandao.
Hata hivyo, washitakiwa wanadaiwa kuwa walituma picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kwa kile kilichodaiwa kwamba mlalamikaji hakutoa fedha alizotakiwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!