Badala yake wametakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika haraka.
Tahadhari hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba, alipotembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea miundombinu ya shirika hilo iliyoharibiwa na tetemeko hilo.
Mramba alisema kuwa kwa sasa wataalamu kadhaa wa Tanesco wanapita katika maeneo mbalimbali kutoa elimu.
"Mtu anaweza kunusurika kwa tetemeko, lakini akapoteza maisha yake kwa kunaswa na umeme na ndiyo maana tetemeko lilipotokea, tulizima umeme haraka hadi tutakaporidhika kuwa kuna usalama," alisema Mramba.
"Tumefika ili kuhakikisha nyumba zote zenye umeme zilizoanguka, nyaya zinaondolewa kwa usalama zaidi, tumeleta mafundi kutoka Mwanza, Geita, Mara na wilaya za mkoa huu ambazo hazijaathirika ili kuongeza nguvu kwa mafundi waliopo."
Alisema wameweka mafundi wote katika hali ya utayari ili watakapohitajika, wafike haraka kutoa msaada.
Aidha, aliwataka wananchi wenye wasiwasi na hali ya umeme katika nyumba zao kutoa taarifa ili wapatiwe huduma ya haraka.
Naye Meneja wa Tanesco mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, alisema hadi Septemba 15, mwaka huu, nyumba 561 zilizoko katika maeneo mbalimbali mkoani humo, zimewekwa salama kwa kuondolewa umeme na kuwa kazi ya kuondolewa umeme katika nyumba nyingine inaendelea.
"Umeme ni muhimu, lakini ni vema mwananchi akakaa hata mwezi mzima bila nishati hiyo kuliko kukaa nao wakati ni hatari kama nyumba ina nyufa," alisema Maze.
Kwa upande wake, fundi mchundo wa Tanesco, Ramadhan Kapele, alisema gharama za kurudisha mfumo wa umeme ndani ya nyumba ikiwamo kutandaza nyaya ni za mteja na kuwa anapokamilisha anapaswa kutoa taarifa katika shirika hilo akiwa na nyaraka muhimu za kitaalamu zinazothibitisha kukamilika kwa kazi hiyo na kuomba kurejeshewa huduma.
"Tukishapata taarifa, tunakwenda kurejesha huduma haraka na bure, maeneo ambayo miundombinu ya umeme imeonekana kuharibika zaidi kutokana na tetemeko, ni Kata za Hamugembe, Rwamishenye, Nshambya na Kashai katika Manispaa ya Bukoba," alifafanua Kapele.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu, alisema wananchi wanaohitaji msaada wa haraka ili kurudi katika mfumo wa kawaida wa maisha yao hadi sasa ni 126,315.
"Tetemeko la ardhi katika mkoa wangu limesababisha nyumba 2,063 kuanguka, nyumba zenye uharibifu hatarishi ambazo hazifai kuishi ni 14,081 na zenye uharibifu mdogo ni 9,471," alifafanua Meja Jenerali Kijuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mkoa.
Alisema hadi sasa kamati ya maafa mkoani humo imekwishapokea msaada wa dawa na vifaa tiba, chakula, mahema, mashuka, mablanketi na vifaa vya ujenzi kama mbao, misumari, mabati na saruji vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 431.7 ambavyo vinaendelea kugawiwa kwa waathirika.
Hata hivyo, baadhi ya waathirika waliozungumza na Nipashe akiwamo Paskazia Gabalanjuna, mkazi wa Omukishenye Kataya Hamugembe, wanalalamika kutopata msaada wowote hata wa chakula kutoka kwa serikali na kwamba wanalazimika kulala nje na familia zao

No comments:
Post a Comment