Ndege hiyo ilikuwa imekaa uelekeo wa kuanza kupaa kwenye njia yake na ndipo wahudumu wakashtuka kuona mmoja wa abiria hakuwa kwenye kiti chake kwa muda mrefu.
Taarifa ambazo Nipashe ilizipata zilisema ndege hiyo aina ya Boeing ilikuwa inajiandaa kupaa jana jioni kwenda Addis Ababa, Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wahudumu hao walipatwa na wasiwasi na kuwaarifu marubani kabla ndege hiyo kuanza kupaa na kisha kuanzisha msako kujua aliko abiria huyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Ramadhani Maleta, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema ndege hiyo ilikuwa inajiandaa kuruka wakati wa tukio hilo.
Baada ya kupata taarifa hizo, marubani wa ndege hiyo walilazimika kuahirisha kuirusha na kuielekeza kwenye eneo la maegesho wakati wakisubiri kujua kinachoendelea.
Alisema wahudumu hao kwa kushirikiana na maofisa wa usalama wa uwanja huo walienda kugonga mlango wa choo cha ndege lakini haukufunguliwa kwa muda mrefu hali ambayo iliwatia wasiwasi.
“Baada ya ndege kuegeshwa watu wa usalama walifika haraka na kuingia kwenye ndege kisha kuanza kugonga mlango wa chooni. Waligonga kama kwa dakika 10 lakini hakufungua na walipokuwa wakitafakari cha kufanya, hatimaye yule abiria alifungua mlango,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Alipofungua walimhoji sababu ya kukaa chooni muda wote huo akawaambia kwamba alikuwa anaumwa tumbo, lakini kutokana na masuala ya kiusalama, hawakumruhusu kuendelea na safari na walimchukua kwa ajili ya kumhoji na uchunguzi zaidi.”
Picha mbalimbali zilizorushwa kwenye mtandao wa Whatsapp zinaonyesha maofisa wa ulinzi na usalama wakiwa wameizingira ndege hiyo baada ya kupata taarifa za abiria huyo.
Hali hiyo iliwafanya abiria kutaharuki kutokana na matukio mengi ya kigaidi ambayo yamewahi kuzikumba ndege na kusababisha vifo vya abiria wote.
Watu waliorekodi tukio hilo na kurusha kwenye mitandao walihoji hatua ya mtu huyo kutaka kufanya tukio wakati ndege haijapaa.
Ingawa haijathibitika iwapo abiria huyo kweli alikuwa mgonjwa au alikuwa na nia mbaya, baadhi ya watu walisikika wakihoji iweje mtu anuie kuteka ndege wakati hata haijapaa.
NIPASHE.

No comments:
Post a Comment