Hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa damu, kutokana na kupokea majeruhi wa ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara katika barabara ya Morogoro.
Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi Goodluck Zelothe, alisema uchangiaji huo utafanyika leo na ni mojawapo ya majukumu ya Zimamoto na Uokoaji na litahusisha askari wote lakini kwa hiari.
“Kutoa damu ni moja ya majukumu yetu, ndiyo maana tumeandaa uchangiaji huu ili kuokoa maisha ya wenzetu,” alisema.
Alisema majukumu mengine ya jeshi hilo, mbali na kuzima moto kuwa ni kuokoa majeruhi wakati wa ajali na kutoa huduma ya kwanza, kuokoa watu wakati wa matukio kama matetemeko ya ardhi, kutumbukia kisimani au shimoni, ajali za vyombo vya usafiri vya angani, majini na barabarani.
Kamanda Zelote alisema pamoja na majukumu yote hayo, bado jeshi hilo lina upungufu mkubwa wa vitendea kazi, yakiwamo magari ya kuzimia moto na kwamba kuna uhaba wa magari sita na wakati yaliyopo ni matatu na hayakidhi mahitaji kulingana na miji katika mkoa huo kukua kwa kasi.
“Mbali na upungufu wa magari ya kuzimia moto pia tuna ukosefu wa gari la uokoaji, gari la wagonjwa na gari maalumu kwa ajili ya kutolea magari yaliyokwama barabarani wakati ajali imetokea,” alisema kamanda huyo.
Pia alisema ujenzi holela katika mkoa huo ni changamoto kubwa inayokwamisha juhudi za jeshi katika kutekeleza majukumu yake kwa kuwa miundombinu ya barabara katika mitaa hairuhusu gari la
kuzimia moto kupita kwa urahisi.

No comments:
Post a Comment