WATU wanne wamehukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mfanyabiasha Seif Athuman na Koplo Josephat Milambo yaliyofanyika katika tawi la NMB tawi la Temeke jijini Dar es Salaam.
Kati ya waliohukumiwa adhabu hiyo, pia yumo muasi wa Jeshi la Burundi, Richard Lucas Muhanza.
Mbali na mwasisi huyo, washtakiwa wengine waliohukumiwa kifungo hicho ni Yusuf Mlete, Isaack Swai na Said Hamisi.
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama Kuu Tanzania na kusomwa na Jaji Salvatory Bongole mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa Jamhuri na sita wa utetezi.
Alisema ushahidi uliotolewa umethibitisha kwamba washtakiwa wanne kati ya sita, wana hatia ya mauaji hayo.
Alisema bila kuacha shaka, Mahakama imeona Anthony Solia na Boniface Makai waliokuwa wakishitakiwa na wenzao, hawana hatia ya mashitaka ya mauaji hayo.
Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo uliongozwa na Mawakili wa Serikali Wakuu, Peter Njike, Bernard Kongola na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo.
Upande wa Utetezi uliongozwa na Mawakili Epholian Kitali na Kaloli Mluge.
Kabla ya adhabu hiyo, upande wa utetezi ulipewa muda wa kujitetea ili washtakiwa wapunguziwe adhabu.
Mawakili hao, kwa nyakati tofauti, walidai kuwa washtakiwa wana familia zinazowategemea na kuomba mahakama iwaonee huruma na kuwapunguzia adhabu.
Hata hivyo, Njike alidai washtakiwa wanastahili adhabu kali kwa kuwa wamekatisha uhai wa watu wawili waliokuwa wanategemewa katika taifa na familia zao.
Alidai kuwa kitendo cha washtakiwa kukatisha uhai wao familia zao zinateseka na kwamba wanastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
“Baada ya mahakama hii kupitia ushahidi wa pande zote mbili, imeona kwamba washtakiwa wanne wana hatia ya mauaji hayo... pia mahakama hii imewaona washtakiwa wawili hamna hatia na inawaachia huru dhidi ya tuhuma za mauaji,” alisema Jaji Bongole.
Washitakiwa walidaiwa kuwa Julai 31, 2009 katika benki ya NMB tawi la Temeke, jijini Dar es Salaam, walimuua Athumani na polisi Koplo Milambo.

No comments:
Post a Comment