Friday, 12 August 2016

Waliokufa kwa sumukuvu wafikia 16




Idadi ya watu waliokufa kwa ugonjwa unaosababishwa na Sumukuvu mkoani hapa imeongezeka kutoka 14 hadi kufikia 16 baada ya mtu mmojakufariki juzi Wilayani Kondoa.



Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Nassoro Mzee alisema jana hadi jana watu 69 walikuwa wameugua ugonjwa katika Wilaya ya Chemba na Kondoa.


“Usiku wa kuamkia jana (juzi) mtu mmoja alikufa kwa ugonjwa huo na kufanya idadi waliofariki kufikia 16.
Kwa mujibu Mkurugenzi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alisema tayari kibali cha tani 100 za chakula kwa ajili ya maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo kimetolewa.
Alifafanua kuwa kati ya chakula hicho, tani 50 zitatolewa kwa mtindo wa kubadilishana.
Alisema tumeziagiza halmashauri zote zilizoathirika na ugonjwa huo zitume taarifa ya chakula ambacho kiko katika kaya zilichoathirika.
“Kibali cha chakula kimetolewa. Hapa nilipo ninaratibu timu yangu ije
huko kuhakiki chakula kilichokusanywa kutoka kwenye familia
zilizoathirika,”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Madunga alisema chakula hicho bado hakijafika.
“Timu yangu bado iko huko vijijini kufanya tathimini kwa watu walioathirika na sumu kuvu hiyo baada ya siku mbili watakuwa wamekamilisha,” alisema Madunga.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!