WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA), umeshatoa notisi kwa wabunge wastaafu 23 kuhama katika nyumba zilizoko Dodoma na kuwapisha wabunge wapya.
Kadhalika, TBA imesitisha ujenzi wa nyumba 10 kila mkoa badala yake zitajengwa nyumba 100 katika mkoa wa Dodoma.
Hayo yalisemwa jana na Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mjini hapa.
Alisema awali TBA ilikuwa na mpango wa kujenga nyumba 10 katika kila mkoa lakini baada ya serikali kufanya uamuzi wa kuhamishia makao makuu yake Dodoma imelazimika kufuta mipango ya awali na kuamua kujenga nyumba zote Dodoma katika eneo la Itega.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso, alisema wakala huo unatakiwa kusitisha ujenzi wa nyumba za mawaziri Jijini Dar es Salaam na badala yake kujenga Dodoma kwa kuwa Rais John Magufuli ameshaamua kuhamia Dodoma, hivyo hakuna sababu ya mawaziri kukaa Dar es Salaam.
Aidha kamati ilishauri serikali kulipa deni la Sh. bilioni 30 inayodaiwa na TBA.
Alisema wakala imekuwa na hali mbaya kutokana na fedha kuwa nje, hivyo wakati umefika kwa wakala kujiendesha kibiashara.

No comments:
Post a Comment