DAR: Idara ya Uhamiaji imewakamata raia wawili wa Congo na Malawi waajiriwa Serikalini. Mmoja alikuwa mfanyakazi wa TANESCO mwingine Mganga Kituo cha Afya Mburahati.
- Raia huyo mmoja wa Congo anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kinyume na sheria za nchi.
Bahilanya Milingita (Congo) alikuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mwingine ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba (Malawi) ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.
Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.
Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kinyume na sheria za nchi.
KWA HISANI YA JMF.
No comments:
Post a Comment