Akizungumza na Nipashe, Kamishna mkazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mohamed Khamis Hamad, alisema wamepokea malalmiko ya kuwapo wahalifu waliokamatwa Zanzibar, lakini wamekwama kufunguliwa kesi.
Alisema kwa mujibu wa Katiba Jeshi la Polisi, majukumu yake ni kuchunguza na kukusanya ushahidi wa kesi na utaratibu wa kufungua mashtaka ni wa Mkurugenzi wa mashitaka Zanzibar.
“Polisi wanalalamika wamekua wakikamata wahalifu na kufanya uchunguzi, lakini majalada ya kesi hayafunguliwi kesi mahakamani na Mkurugenzi wa mashitaka,” alisema.
Hata hivyo, alisema kutokana na uzito wa jambo hilo, Tume imeamua kuchukua hatua ya kukutana na Mkurugenzi wa mashtaka kutafuta ukweli wa tatizo hilo.
Alisema polisi wanalazimika kukaa na wahalifu muda mrefu bila ya kufunguliwa mashtaka na wakati mwingine kulazimika kuachiwa kwa dhamana.
Hamad alisema kitendo cha polisi kukaa na mtuhumiwa kwa zaidi ya saa 24 bila ya kumfikisha mahakamni ni kinyume na misingi ya utawala wa sheria.
Alisema kabla ya kufungua kesi mahakamani kuna mambo mengi yanahitaji kuzingatiwa ikiwamo ushahidi kujitosheleza dhidi ya mtuhumiwa.
Alisema kuna umuhimu mkubwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee na Jeshi la polisi kuwa na vikao vya ushirikiano vya mara kwa mara kufanikisha majukumu yao.
Alisema Tume baada ya kukutana na DPP wa Zanzibar, watatoa mapendekezo yao serikalini juu ya hatua za kuchukua katika mvutano huo ili kuhakikisha wahalifu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa wakati muafaka.
Alisema kitendo cha kumuweka mtuhumiwa mahabusu bila kumfikisha mahakamni kwa zaidi ya siku 20 ni kinyume na misingi ya utawala wa sheria na haki za binadamu.
Majalada yaliyokwama kufunguliwa kesi Mahakamni pamoja na majalada kukabidhiwa Mkurugezi wa mashitaka Zanzibar pamoja na jalada la kesi dhidi ya Katibub Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wengine ambao majalada yao hayajafikishwa mahakamni ni aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani, Hija Hassan Hija na watuhumiwa wa kuhusika na milipuko ya mabomu Zanzibar.

No comments:
Post a Comment