Saturday, 20 August 2016

Simba mla watu azua taharuki Songwe


WANANCHI wa kitongoji cha Kikamba, Kijiji cha Itizilo, Chunya mkoani Songwe, wamepatwa na taharuki huku wengine wakiyakimbia makazi yao, baada ya simba kumuua na kumla nyama mtoto Shija Majaliwa (3), mkazi wa kijiji hicho.





Simba huyo anayesadikika kuishi kwenye mashamba ya wakazi wa vijiji vilivyoko kwenye kata hiyo, alimvamia na kumuua mtoto huyo ambaye alikimbia baada ya wanakijiji kupiga mayowe kuomba msaada wakati akijiandaa kumtafuna.
Majaliwa Ninchilo, baba mzazi wa Shija, alisema mtoto wake alikamatwa na mnyama huyo saa nane usiku, akiwa shambani, nje kidogo ya nyumba hiyo kulinda mazao.
Alisema walifikia hatua ya kulinda mazao yao nyakati za usiku baada ya tembo kuvamia mashamba wanakijiji hao. Alisema wakiwa lindoni hawakufunga mlango wakijua hakuna jambo baya linaloweza kutokea.
Ninchilo alisema wakiwa lindoni na silaha za kijadi, walisikia kishindo kikubwa cha mlango ukifunguliwa na kuamua kurejea ndipo walipomkuta mtoto ameuawa na simba ambaye alikuwa amemla baadhi ya viungo vya mwili wake.
Hata hivyo, alisema simba huyo alikimbilia porini na mabaki ya mtoto huyo. Alisema walishirikiana na mumewe kupiga mayowe na majirani kufika na kukuta janga hilo.
Kutokana na hali hiyo, wakazi wa kijiji hicho walimsaka simba huyo lakini hawakufanikiwa kumpata.
Donald Maganga, Diwani wa Ngwala (CCM) alikiri kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa shughuli za maendeleo zimesimama kutokana na hofu ya kuvamiwa na kudhuriwa na mnyama huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathius Nyange, alikiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba jeshi lake kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa watakutana kujadili namna ya kukabiliana na simba huyo huku wakiruhusu familia ya kuendelea na maziko ya mabaki ya mtoto huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alisema ameshitushwa na tukio hilo na kusema wanajipanga kufika eneo hilo kuzungumza na wakazi, ikiwa pamoja na kuwataka wawe makini na watoto nyakati za usiku ili kuzuia vifo vinavyotokana na kuvamiwa na wanyama

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!