Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Siku ya Vijana Duniani, Waziri Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Moudline Castico, alisema Serikali ya Zanzibar imeshakaa na ubalozi wa Oman na nchi zingine kuondoa matatizo yaliyojitokeza ya udhalilishaji.
Alisema vijana wengi wanaokutana na matatizo ya udhalilishaji ni wale wanaondoka kwa njia za panya bila ya kufuata taratibu za safari kutoka serikalini, hivyo kuwataka vijana kuhakikisha wanaondoka nchini kwa kufuata taratibu ili wanapopatwa na matatizo, serikali iwasaidie.
“Ni kweli baadhi ya vijana hasa wanawake wanaokwenda kufanya kazi za ndani Oman na Muscat, huwa wanafanyiwa vitendo vya udhalilishaji na waajiri wao huwanyang’anya hati za kusafiria ili wasiweze kurudi wanapodhalilishwa.
Aidha, alisema licha ya kudhalilishwa na kunyanyaswa kijinsia, alisema vijana kutoka Zanzibar ni wavivu wa kufanya kazi na kuwapa wakati mgumu waajiri wao.
Alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Kampuni za Uwakala wa Ajira Zanzibar, imewaunganisha vijana 498 kwenda kufanya kazi Oman, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia.
Alisema vijana hao wameajiriwa kwa nafasi za kazi za udereva, saluni, hoteli, upishi, kazi za nyumbani, ubaharia, taasisi za fedha, viwandani na ulinzi katika sekta binafsi.
Hata hivyo, alisema bado kuna wimbi kubwa la vijana Zanzibar ambao hawana ajira pamoja na juhudi za serikali za kuwajengea uwezo wa kujiajiri kupitia sekta isiyo rasmi.
Castico alisema serikali chini ya mpango huo, imefanikiwa kutoa mikopo 337 yenye thamani ya Sh. milioni 523.4 na kuwanufaisha wananchi 1,907 katika visiwa vya Unguja na Pemba.

No comments:
Post a Comment