Sunday, 28 August 2016

Saudia: Amuua daktari wa kiume kwa kuuona utupu wa mkewe wakati wa kumzalisha



IYADH, Saudi Arabia
POLISI nchini Saudi Arabia wamemkamata mwanamume mmoja aliyempiga risasi mwanaume mtaalamu wa afya ya uzazi aliyemsaidia mkewe kujifungua mtoto akisema ni haramu kwa mwanamume kuona sehemu za siri za mkewe.




Inasemekana kuwa mshukiwa alikasirishwa na wasimamizi wa hospitali waliomruhusu daktari Muhannad al Zabn kumsaidia mkewe kujifungua.

Shirika la habari la Gulf News lilisema mshukiwa alitaka mkewe ahudumiwe na mtaalamu wa kike akidai desturi ya jamii yake ni kwamba mwanamume hafai kuona uchi wa mwanamke ambaye si mkewe, hata kama yeye ni daktari.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!