Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ambayo mwaka huu inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara sambamba na sherehe za miaka 80 ya klabu hiyo, ambayo itaadhimishwa siku ya Simba Day August 8 2016, leo August 5 2016 imetangaza kuingia mikataba na mastaa watano wa kimataifa.
Simba ambao wameingia mikataba na mastaa hao akiwemo mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi waliyemuwinda kwa zaidi ya misimu miwili Laudit Mavugo, wamefanikiwa kuwasajili pia Fredric Blagnon kutokea Ivory Coast, Musa Ndusha, Janvier Bokunguna Method Mwanjale.
Mastaa wote wa kimataifa waliosajiliwa na Simba watatambulishwa rasmi siku ya Simba Day August 8 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
No comments:
Post a Comment