- Matumizi ya mili.900/= yawaponza
MKURUGENZI wa zamani wa Mamlaka ya Vitambusho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake saba wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, pamoja na wenzie nane Avelin Momburi, Benjamin Mwakatumbula, Joseph Makani, Astery Ndege, George Ntalima, Sabina Raymond na Xavery Kayombo wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam jana.
Wakikabiliwa na mashtaka 27 zikiwamo tuhuma za kuhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh. milioni 901.
Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Avelin Momburi, Benjamin Mwakatumbula, Joseph Makani, Astery Ndege, George Ntalima, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa akisaidiana na waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, Janeth Machulya, Joseph Kiula na Fatuma Waziri.
Upande wa utetezi uliongozwa na jopo la mawakili wa kujitegemea, Michael Ngalo, Jonson Jamhuri, Seni Malima, Godwin Nyaisa, Esaria Mosha, Godian Njaala na Silvester Kakobe.
Maimu ambaye anakabiliwa na mashtaka 16 kati ya 27, alisomewa mashtaka hayo jana saa 7:12 mchana pamoja na wenzake katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo uliokuwa umefurika watu wanaodaiwa kuwa ndugu wa washtakiwa hao.
Mbagwa alidai kuwa katika shtaka la kwanza hadi la nne siku, tarehe na mwaka tofauti Maimu na Mwakatumbula wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kuruhusu malipo kwa kampuni ya Gotham International Limited (GIL) ya Dola za Marekani milioni 2.7 bila kutumia kiwango cha kubadilishia fedha kilichowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kusababisha kampuni hiyo kujipatia Sh. 124,976, 676.76.
Katika shtaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 15, mwaka 2010 na Mei 16, mwaka 2015 katika ofisi za Nida, Maimu na Mwakatumbula wakiwa watumishi wa umma kwa kutumia madaraka yao, waliruhusu malipo ya Dola za Marekani bila kutumia kiwango cha kubadilisha fedha kilichowekwa na BoT na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 167,445,676.76.
Mbagwa alidai katika shtaka la sita, Aprili 16, mwaka 2012 katika Makao Makuu ya Nida, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ndege alighushi nyaraka akionyesha kampuni ya Aste Insurance Brokers Company Limited inastahili kulipwa Sh. milioni 22.5 kwa ajili ya huduma ya bima huku akijua amepotosha.
Ilidaiwa kuwa kati ya Februari 22 na Aprili 17, mwaka 2012 katika ofisi za Nida, Momburi, Mwakatumbula na Ntalima wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kuruhusu malipo ya Sh. 22,582,281 kwa kampuni ya Aste Insurance Brokers Company Limited na kusababisha kampuni hiyo kujipatia isivyo halali fedha hizo.
Swai alidai kuwa Agosti 29, mwaka 2012 katika ofisi za mamlaka hiyo kwa nia ya kumdanganya mwajiri wake, Ndege alighushi nyaraka kwamba kampuni ya kushughukia bima inastahili kulipwa Dola za Marekani 460,000 huku akijua siyo kweli.
Upande huo wa Jamhuri ulidai kuwa kati ya Mei 29 na 31, mwaka 2012 katika ofisi za Nida, Mshtakiwa Maimu, Mwakatumbula na Makani walitumia madaraka yao vibaya kwa kuruhusu malipo ya Dola za Marekani 11,000,000 kwa Kampuni ya Iris Corporation Berhad na kusababisha kampuni hiyo kujipatia fedha hizo.
Machulya alidai kuwa kati ya Juni Mosi na 6, mwaka 2013 katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, mahali pasipofahamika ndani ya ofisi hiyo, mshtakiwa Mwakatumbula, Ntalima na Kayombo walikula njama ya kutenda kosa kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Aliendelea kudai kuwa kati ya Novemba 4, mwaka 2011 na Aprili 30, mwaka 2012, Maimu na Raymond katika makao makuu ya Nida, wakiwa watumishi wa umma, waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 901,078,494.
Kwa mujibu wa mashtaka yanayowakabili ya kuhujumu uchumi, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi pale upelelezi utakapokamilika. Kesi hiyo itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania au mahakamani hapo ikiwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini akitoa kibali hicho.
Mbagwa alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na haukuwa na pingamizi la dhamana kwa washtakiwa lakini kwa kuwa mashtaka hayo thamani ya fedha wanazodaiwa kuhujumu ni zaidi ya Sh. milioni 10, mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa dhamana hadi Mahakama Kuu.
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa mshtakiwa wa pili na wanne, mashtaka yao hayahusiani na uhujumu uchumi, na uliomba mahakama kutoa dhamana dhidi yao.
Hakimu alisema atatoa uamuzi kesho wa ama kuwapa dhamana au la mshtakiwa wa pili na wa nne, kesi hiyo itatajwa Agosti 31, mwaka huu na washtakiwa wapelekwe mahabusu.
BAADA YA KUSOMWA MASHTAKA
Baada ya washtakiwa hao kuamriwa kurudishwa mahabusu, wanaodaiwa kuwa ndugu wa washtakiwa waliangua kilio nje ya mahabusu ya mahakama hiyo huku wakihoji watalala mahabusu mpaka lini.
Nipashe:

No comments:
Post a Comment