Monday, 29 August 2016

Mtoto mwenye betri moyoni kurudi shule

Happiness John (5), aliyefanyiwa upasuaji Julai 15 na kuwekewa betri ndani ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), anatarajia kuanza tena masomo Septemba 12 shule itakapofunguliwa.


Happiness John (5).

 

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, mama wa mtoto huyo, Elitruda Malley alisema mwanaye anaendelea vyema kiafya kiasi kwamba atarejea shule hivi karibuni.
"Anaendelea vizuri kabisa... namshukuru Mungu," alisema Malley ambaye alikabidhiwa na JKCI jukumu la kumuangalia kwa karibu.
"Nimeshaanza kazi (na) Happiness naye atarudi tena shule tarehe 12 Septemba mara baada ya shule yao kufunguliwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!