Friday, 19 August 2016

MSAADA WA KWANZA PASIPO NA MAPIGO YA MOYO



Unaweza kuweka vidole shingoni kuhisi mapigo ya moyo, kama ilivyooneshwa chini ya Pumzi maalum ya kuokoa maisha. Au sikilizia upande wa 2 kifuani, penye alama ya X

Kama hakuna mapigo ya moyo, jaribu kuanzisha upumuaji kwa kutumia mibinyo kifuani kwa kubinya na kuachia. Ni muhimu kuanzisha mibinyo kifuani haraka, hivyo kama huna uhakika kuwepo mapigo ya moyo, au kama mapigo ya moyo ni dhaifu mno, ni salama zaidi kuanzisha mibinyo kifuani.








Mpatie mibinyo kifuani
Sukuma sana na harakaharaka katikati kifuani mara 30. Sukuma chini moja kwa moja, angalau uingie sentimeta 5 (inchi 2) ndani. Jaribu kwenda haraka zaidi, angalau mara 100 kwa dakika, lakini kiwango bayana siyo muhimu. Sukuma kwa nguvu na haraka!
Toa pumzi za kuokoa maisha
Baada ya mibinyo 30 kifuani, toa pumzi za kuokoa maisha 2 ambazo zitasababisha kifua kuinuka.
Endelea na mibinyo na pumzi za uokoaji
Endelea kufuatisha mibinyo kifuani na pumzi za kuokoa maisha –baada ya kila mibiny 30 kifuani toa pumzi 2 za uokoaji. Unaweza kutakiwa kulifanya zoezi hili kwa muda mrefu. Endelea hadi mgonjwa atakapoanza kupumua na kuwa timamu kiakili, au hadi kutakapokuwa hakuna shaka kuwa yu hai.
Tafuta msaada
Kama unaweza kumfikisha hospitalini haraka, fanya hivyo. Endelea kumfanyia mibinyo kifuani na pumzi za uokoaji njiani mkielekea hospitalini. Hii itasaidia kuendeleza utendaji wa viungo vya mwili hadi utakapopata msaada.


Hii inaweza kumurudishia mtu uhai baada ya kupigwa na umeme, kuzama majini, kama amepigwa na kitu kikubwa kifuani, baridi kali, au kutumia kiasi kikubwa cha dawa kuliko kinachohitajika.
Mibinyo kifuani siyo rahisi kumsaidia mtu ambaye amepata mshituko wa moyo, lakini ni bora kujaribu, hasa kama unaweza kupata msaada zaidi wa kitabibu. (Angalia zaidi juu ya Mshituko wa moyo.)
Kuna kifaa (defibrillator) ambacho kinaweza kutoa umeme mdogo kwa ajili ya kuushitua moyo kuanza kufanya kazi tena baada ya kupatwa na tatizo la mshituko wa moyo. Ulizia kama kifaatiba hicho kinapatikana eneo katika lako na wapi kabla ya ajali haijatokea. Wakati mwingine hupatikana kwenye gari za kubebea wagonjwa, au katika sehemu za huduma kwa umaa kama vile hoteli kubwa.

Via-Hesperian health guides.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!