Kitengo cha damu salama katika hosipitali ya taifa ya muhimbili kimewataka Watanzania wanaochangia damu katika kitengo hicho kwenda kuchukua majibu ya damu ili kuendelea kujiweka katika mazingira ya afya.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na afisa mhamasishaji mkuu wa damu salama katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili Dkt. Hamis Kubinga wakati akiongoza zoezi la uchangiaji damu kwa wanachama wa chama cha wamiliki wa duka za dawa muhimu mkoa dar es salaam waliposhiriki kuchangia damu leo.
Kwa upande wa wananchi na wanachama waliojitokeza kuchangia damu leo jijini Dar es salaam wametaka elimu zaidi iendelee kutolewa kwa wananchi ili kufahamu na kuondoa woga kuhusu usalama na siri zao za kiafya kwa jamii pindi wanapojitokeza katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment