Mimi nataka niongelee hii kero ya omba omba kwenye sekta ya utalii. Hivi ni nini dawa yake? Watalii wengine wamejichangisha vichele vyao kwa miaka kadhaa ili waje watembelee maajabu ya Tanzania wanaanza kuombwa kila kona. si hotelini, ni tip, housekeeping tip, dereva wa magari ya mbugani tip mwisho wake baada ya safari kuwa ya kufurahia wanaanza kuchukia na kuogopa.
Wafanyakazi wengine wa Utalii hata haya hawana wanakwenda kwa watalii kulia shida ooh my sister needing medical help in India operation help me. Jamani haya ni maisha kweli? Mbona aibu. Watalii hao hao wakienda Kenya au Uganda hawaombwi hata senti. Sasa sijui sisi vipi? mimi naona hili ni Jipu hasa lifanyiwe kazi na wahusika.
Mdau:
No comments:
Post a Comment