ILI kufanikiwa kwenye jambo lolote maishani na kulifanya vizuri ni lazima ujifunze, upate maarifa sahihi ambayo yatakuwezesha kuchukua maamuzi sahihi yatakayokuletea matokeo bora.
Leo tutazungumzia kanuni tatu muhimu za fedha, ambazo huenda hujawahi kufundishwa popote.
Kwa kujifunza kanuni hizi na kuzifanyia kazi, maisha yako kifedha yanaweza kubadilika na utaanza kuona mambo mazuri yakitokea kwenye maisha yako.
Kanuni ya kwanza; Kutengeneza fedha.
Kanuni hii inasema kwamba UTALIPWA KULINGANA NA THAMANI UNAYOZALISHA.
Hii ina maana kuwa ili ulipwe fedha ni lazima utoe thamani, ni lazima ufanye kitu ambacho kinawafaidisha wengine na wao wawe tayari kulipia kile ulichofanya.
Iwe ni kazi au biashara huwezi kutengeneza fedha bila wewe kwanza kutoa fedha au thamani ya huduma kulingana na thamani ya fedha.
Kanuni hii ni rahisi sana kwa sababu kama unataka kupata fedha, angalia wengine wanataka nini wapatie na kama unataka kupata fedha zaidi ya unavyopata sasa, ongeza thamani ya kile unachofanya sasa.
Kama unahudumia watu watano, hudumia watu kumi, tayari utakuwa umeongeza wigo wako wa kupata fedha zaidi.
Bahati nasibu, kamari(betting), au njia nyingine zote ambazo zinakutamanisha kupata fedha bila ya kutoa thamani, ni maigizo na utaishia kupoteza fedha au kutapeliwa.
Kanuni ya pili; Hifadhi/tunza fedha.
Watu wengi baada ya kutengeneza fedha huwa wanakimbilia kutumia bila ya kuwa na mpangilio maalumu.
Unapata fedha na kukimbilia kununua vitu ambavyo unafikiri ni muhimu wakati sio muhimu.
Wengi wetu kila wapatapo fedha wanasukumwa kuitumia zaidi, matatizo ndio hujitokeza, marafiki wanaongezeka, wengine ndio muda wa kuongeza wake ama nyumba ndogo.
Hivyo unapopata kipato chako, kabla hujakimbilia kufanya matumizi au hata uwekezaji, kitunze kwanza, kaa nacho kwanza, kiweke kama akiba benki, japo kwa kipindi fulani.
Halafu katika kipindi hicho ambacho unatunza hicho kipato chako, endelea na maisha yako kama vile huna fedha ile.
Yaani endelea na maisha yako bila ya kufikiria kwamba una fedha benki ambazo unaweza kutumia kwenye kitu chochote unachotaka.
Kwa mfano kuna kitu unatamani sana kununua, na ungeweza kununua kwa fedha uliyopata, ila hufanyi hivyo kwa sababu fedha hiyo ipo kwenye hatua ya kutunzwa.
Hata kama inakubidi kushinda njaa, fanya hivyo, lakini fedha ile uwe umeitunza.
Unaweza usielewe vyema ninachosema hapa, lakini kwa kifupi ninachotaka hapa ni ile nidhamu ya wewe kuweza kuiendesha fedha na sio kuacha fedha ikuendeshe wewe.
Kwa sababu watu wengi wanapokuwa na fedha ni kama akili zao zinaacha kufanya kazi mpaka fedha ile iishe.
Nafikiri umewahi kukutana na kauli hizi, mimi nikipata fedha siwezi kutulia mpaka fedha hiyo iishe, au ukiwa huna fedha unakuwa na mawazo mazuri sana, lakini ukishazipata mawazo yote yanapotea.
Kanuni ya tatu; Ifanye fedha ikuzalishie.
Baada ya kutengeneza fedha (kanuni ya kwanza) na kuweza kuitunza (kanuni ya pili), sasa unahitaji kuifanya fedha yako kukuzalishia.
Hapa unaiweka fedha yako sehemu ambapo inazalisha faida zaidi ya kipato unachopata sasa.
Kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza kuifanya fedha yako ikuzalishie zaidi.
Baadhi ya sehemu hizo ni; Kuanzisha au kuendeleza biashara uliyonayo, kuwekeza kwenye mali, kama ardhi na nyumba ambazo utazitumia kuingiza kipato, kuwekeza kwenye masoko ya fedha kama kununua hisa, vipande na kadhalika.
Sehemu yoyote unayoweka fedha yako, hakikisha kuna faida zaidi unapata, kwa sababu kuna sehemu ambazo watu huwa wanafikiri wamewekeza, lakini ukweli ni kuwa wanapoteza fedha.
Baadhi ya sehemu hizo ni kama, kuweka fedha benki kwa kuamini unapata riba, kununua vitu vya matumizi kama magari ya kutembelea, ukiamini ukiwa na magari mengi ya kutembelea ni mali zinazokuzalishia.
Hizi ndizo kanuni tatu muhimu za fedha unazotakiwa kuzijua na kuishi nazo kila siku.
Huenda ulikuwa unazitumia lakini ulikuwa hujazijua vizuri, sasa umeshazijua, hivyo ishi nazo na usijaribu kuvunja hata moja.

No comments:
Post a Comment