Dodoma ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo chenye reli ya kati na karakana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja la mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59
. Dodoma ni mji wa Tanzania ya kati. Imetangazwa kuwa mji mkuu waTanzania mwaka 1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia ikulu halisi ya rais. Lakini bungehukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma.
Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna Wangulu na piaWasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale hukoZimbabwe au Afrika Kusini. Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.
Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 2,083,588 mwaka 2012. Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga, maharagwe na alizeti, pamoja na mifugo na kuku.
Asili ya jina
Mkoa wa Dodoma uko katikati ya Tanzania umepakana na mikoa yaManyara, Morogoro, Iringa na Singida. Sehemu kubwa ya eneo lake ninyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.
Wilaya ya Bahi, Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Kondoa, Wilaya ya Kongwa, Wilaya ya Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 2,083,588.
Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki palepale
Mawasiliano
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodomakwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.
No comments:
Post a Comment