WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kuingiza mafuta nchini.
Alisema kwa sasa kampuni zinazojishughulisha na uingizaji mafuta ni chache.
Kutokana na maelezo ya Proesa Muhongo, utekelezaji wa haraka wa hatua hiyo pamoja na mambo mengine, utaongeza ushindani wa kibiashara na hatimaye kusaidia kupunguza bei ya bidhaa hiyo hapa nchini.
Alitoa ushauri huo jana wakati wa ziara yake jijini hapa alipotembelea Bohari ya Kampuni ya GBP, inayohusika na upokeaji mafuta kupitia bandari ya Tanga na kisha kuyasambaza katika mikoa mbalimbali nchini.
“Bei ya mafuta yanayouzwa nchini imekua ghali ikilinganishwa na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBP, Badar Masoud, akitoa taarifa kwa Waziri Muhongo alisema, uamuzi wa serikali kupitisha shehena ya mafuta katika bandari ya Tanga umerahisisha upatikanaji wa bidhaa hiyo na kuondoa adha ya msongamano kwa baadhi ya wasafirishaji wanaolazimika kwenda Dar es Salaam ili kuyapakia.
“Ombi langu kwako ni kuwa serikali ipange bei elekezi ya kuuza bidhaa hii hasa kwa mikoa yote ambayo inaunda Kanda ya Kaskazini ili kuleta usawa sokoni,” alisema.
No comments:
Post a Comment