MLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), inatarajia kuvunja zaidi ya nyumba 1,000 ambazo zimejengwa katika hifadhi ya reli na miliki zingine za ardhi ya mamlaka hiyo.
Ofisa Uhusiano wa Tazara, Regina Tarimo, alisema jana kuwa kazi ya kuzitambua na kuweka alama nyumba ambazo zinatakiwa kubomolewa kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma mkoani Songwe, ilifanyika kati ya mwaka 1998 na 2000.
“Kwa kipindi hicho, kulikuwa na nyumba 700 ambazo zilitakiwa zibomolewe, ila kwa sasa ziko zaidi ya nyumba 1,000 ambazo zimewekewa alama kwa ajili ya kubomolewa,” alisema.
Alisema mbali na kutoa tangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu ubomoaji huo ambao utafanyika baada ya siku 60 kwa gharama za waliojenga, wamewaandikia Wakurugenzi wa Wilaya, Makatibu Tawala na Maofisa Ardhi wa Wilaya mbalimbali ambako reli imepita, kuwajulisha kuhusu azma hiyo.
Alitaja maeneo ambayo viongozi wake wamewaandikia barua kuwa ni Ilala, Temeke, Kilombero, Njombe, Mbeya, Mbarali na Mbozi.
Tarimo alisema kwa wale watakaokuwa na nyaraka halali, fidia itategemeana na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kulipwa fidia.
Alitaja maeneo ambayo yana wavamizi wengi kuwa ni Kurasini-Yombo, Yombo-Dar es Salaam Karakana, Yombo- Dar es Salaam, Yombo-Mwakanga, Mangu’ula, Ifakara, Mlimba, Makambako, Mbeya, Mbalizi na Tunduma.
Aidha, alisema Tazara inawakumbusha wananchi kuwa ni hatari kujenga kwenye hifadhi ya reli au miliki nyingine.
Tazara ilitoa tangazo Jumatano ya wiki hii kwenye vyombo vya habari ambalo limetoa siku 60 kwa wavamizi wa miundombinu ya reli ya mamlaka hiyo kubomoa majengo yao na kwamba baada ya muda huo kupita, ubomoaji utafanyika kwa gharama za wahusika.

No comments:
Post a Comment