Wednesday, 24 August 2016
ARUSHA: Mwanamke aliyechoma nyumba yake na maduka 3 baada ya kutofautiana na mumewe, amefariki kwa kujinyonga na nguo akiwa mahabusu.
August 21 2016 ziliripotiwa habari za mama mmoja anayejulikana kwa jina la Victoria Edward Wenga kuchoma moto maduka matatu na nyumba yake ya kuishi katika kata ya Lemara Arusha. Chanzo cha mama huyo kuchoma moto ilidaiwa ni ugomvi uliokuwepo kwenye familia kati ya mama huyo na mume wake anayejulikana kwa jina la Edward Wenga.
Habari nilizozipokea muda si mrefu zinasema kwamba mama huyo amejinyonga kwa kutumia nguo yake na kufariki dunia. Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amesema alijinyonga akiwa kituo cha polisi kama mahabusu ambapo polisi walipata taarifa baada ya mahabausu wenzake kupiga kelele.
Chanzo: Millard Ayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment