Meneja Miradi ya Afya wa Amref Kanda ya Ziwa, Dk. Benatus Saambili, akizungumza baada ya Kiongozi wa Mbio za
Mwenge Kitaifa, George Mbijima, kuzindua miradi ya majengo hayo, alisema majengo hayo yamekarabatiwa na mengine kujengwa na shirika hilo kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Idadi ya Watu (UNFPA).
Dk. Saambili alisema Amref ilijenga vituo vya afya kwa huduma ya wazazi wajawazito Iyovu wilayani Bukombe, Bwanga (Chato) na Iboya (Mbogwe), kwa ajili ya kupeleka huduma kwa wananchi.
Alisema shirika hilo linashirikiana na serikali katika masuala ya afya kwa lengo la kuwafikishia wananchi hasa waliopo vijijini huduma bora za afya.
Alifafanua kuwa jengo la Bwanga limegharimu Sh. milioni 301 huku jengo la uzazi na upasuaji la Kituo cha Afya Iboya lililopo wilayani Mbogwe likigharimu Sh. milioni 380.
Awali, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bwanga, Dk. Deogratias Rubanzibwa, alisema mradi wa jengo la huduma ya upasuaji kituoni hapo ulianza kutekelezwa Januari, mwaka huu, ili kuepukana na wananchi kwenda umbali wa kilomita 60 kuifuata hospitali ya wilaya.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Iboya, Dk. James Malashi, alisema wanashukuru kwa shirika hilo kukamilisha ujenzi wa jengo hilo licha ya kutopata vifaa.
Kiongozi wa Mbio wa Mwenge Kitaifa, George Mbijima, akizindua majengo hayo aliwataka wananchi kuyatumia na kuyatunza kwa lengo la kuboresha afya zao.

No comments:
Post a Comment