Wednesday 10 August 2016

Aachiwa huru baada ya kufungwa miaka 30



Arusha. Mahakama ya Rufani imemfutia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, Johnson Ashraf mkazi wa Mererani, ambaye alikuwa amefungwa kwa kosa na ujambazi wa kutumia silaha.


Ashraf alitiwa hatiani na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha baada ya kutuhumiwa Mei 31 mwaka 2005, akiwa na wenzake saa tisa usiku walivunja nyumba na kuiba vitu vyenye thamani ya Sh 8.1 milioni mali ya Dismas John kwa kutumia silaha.
Majaji watatu wa mahakama ya rufani, Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Angela Kileo na Jaji Salum Masati walitoa maamuzi hayo baada ya kupitia rufani ya mtuhumiwa huyo na ushahidi wa pande zote.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!